IQNA

Jinai za Israel

Israel yawazuia  waumini wa Kiislamu kusali katika Msikiti wa Al-Aqsa

21:11 - January 19, 2024
Habari ID: 3478216
IQNA - Maelfu ya waumini wa Kiislamu walizuiliwa na jeshi katili la utawala wa Kizayuni wa Israel kuingia katika Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) kwa ajili ya kuswali swala ya Ijumaa.

Kwa mujibu wa Idara ya Wakfu ya Kiislamu, chombo cha Jordan kinachosimamia eneo hilo takatifu, ni waumini 15,000 pekee walioruhusiwa kuingia katika uwanja wa Msikiti wa Al-Aqsa Mashariki mwa al-Quds kwa ajili ya Sala ya Ijumaa, shirika la habari la WAFA la Palestina limeripoti.

Utawala wa kikoloni wa Israel uliweka vikwazo vikali kwa Wapalestina kuingia katika msikiti huo, ambao ni wa tatu kwa utakatifu katika Uislamu.

Idara ya Wakfu ilisema kuwa Israel iliweka vizuizi karibu na Mji Mkongwe wa al-Quds na kuwazuia maelfu ya waumini kufika msikitini. Wengi wao walilazimika kusali nje ya boma baada ya kuzuiwa na majeshi ya Israel.

Vizuizi hivyo vimewekwa tangu Oktoba 7, wakati Hamas ilipoanzisha mfululizo wa mashambulizi ya roketi dhidi ya Israel, ambayo ililipiza kisasi kwa mashambulizi mabaya ya anga na ardhini kwenye Ukanda wa Gaza. Mzozo huo umesababisha vifo vya zaidi ya Wapalestina 24,600, wengi wao wakiwa raia na kujeruhi makumi ya maelfu ya wengine.

Utawala wa Israel pia uliwakandamiza waandishi wa habari waliokuwa wakiandika habari kuhusu hali ya mji wa al-Quds na kutumia maji ya pilipili kuwatawanya waumini wa kitongoji cha Wadi al-Joz kilicho karibu.

Hatua hizo za Israel zimezua hasira na mfadhaiko miongoni mwa Wapalestina wanaouona Msikiti wa Al-Aqsa kuwa alama ya utambulisho wao wa kidini na kitaifa.

3486868

Habari zinazohusiana
captcha